WANAUME WENGINE SIJUI WAKOJE


Hii simulizi nimepewa na rafiki yangu, huyu rafiki yangu alikutana na kaka mmoja hivi huko kwenye Internet basi wakawa wanaendelea kuchat na kubadilishana mawazo, basi ikafikia wakati wakaamua kubadilishana namba za siku. basi wakawa wanawasiliana kwa kupigiana simu na kutumiana msg mara kwa mara. kumbe yule kaka nia yake ya kuwa huko Marafiki ni kutafuta msichana wa kuwa nae na huyu dada yeye anaboyfriend wake ila alikuwa anatafuta marafiki tu wa kawaida kwa ajili ya kubadilishana mawazo.


Basi siku moja yule kaka akamwambia yule dada kuwa wakutane sehemu ili wajuane , yule kaka akamwabia yule dada aende Magomeni kwenye hotel fulani hivi lakini yule dada akamwambia yule kaka kuwa hataweza kwenda sehemu hiyo labda wakutane sehemu iliyowazi ( Bar) basi yule jamaa akakubali, wakaongea yule kaka akajielezea yeye kuhusu maisha yake na dada nae akamwambia yule kaka. basi baada ya saa moja yule dada akaaga kuondoka, basi wakaachana kila mtu akaenda zake kwao. yule kaka akaanza kumwandikia yule dada kuwa anampenda anataka awe mke wake, basi yule dada akamwambia kuwa me tayari nina rafiki wa kiume basi huyo kaka anasema pls me nakupenda sana hata leo niko tayari kukuoa sasa yule dada akamwambia wewe utampendaje mtu kwa siku moja tu baada ya kumwona na hata hujui tabia yake? akasema tabia tutajuana tu, basi yule dada akamwambia sitaweza kuwa na wewe kwani tayari nina mtu. basi bwana yule kaka akawa anapiga simu hadi inakuwa kero, basi yule dada akaona bora amwambie boyfriend wake basi siku moja yule kaka akapiga simu ikapokelewa na boyfriend wa yule dada akamuuliza unataka nini yule kaka akasema mwenye simu hiyo akajibiwa hata me ni mwenye simu kwani ni ya mchumba angu. basi yule kaka akakata simu. baada ya muda akapiga tena yule dada akamwambia we kaka samahani sana nadhani nimekwambia kuwa ninamtu na wala wewe sikuhitaji, akaniambia hunipendi kwa sasabu ni mweusi? au kwa kuwa me Maskini? baada ya hapo yule kaka akaanza kumtukana yule dada eti kwanza huna lolote wewe, sura mbaya, mwembamba na maneno kibao, anatuma msg za matusi kibao? anamwambia huyu dda mimi nina nyumba na gari hapo mwenge wala sio maskini kama nilivyokwmbia, na nimesoma nina Masters na nina kazi nzuri. sasa swali langu ni kwamba hivi mtu ukimkataa ndo akutukane??? alivyokuwa anakutaka hakujua kama wewe ni mbaya? habari ndo hiyo wapendwa.

1 comment:

Anonymous said...

Huyo kaka kwa kweli ni mshamba na mjinga. hajui kuwa mapenzi hayalazimishi? maneno ya mkosaji hayo