janal nilikuwa naangalia Channel ten kipindi cha ' Je Tutafika' ambacho kinaendeshwa na Mzee Makwaiya wa kuhenga. alikuwa ameenda nchi ambayo inaitwa Sumaliland, yaani sijawahi hata siku moja katika maisha yangu kusikia nchi inayoitwa kwa jina hilo zaidi ya kujua kuwa kuna nchi inayoitwa Somalia.
Kwa jinsi nilivyoona katika TV ianelekea nchi hiyo ina amani sana kwani hela zinabadilishwa tu hadharani, zinabebwa kwenye Mikokoteni, Yaani wabadilisha hela wako sokoni tena wameweka hela zao chini tu na watu kibao wanapita. Yaani ukifika muda wa kwenda kuswali wanaacha hela zao hapo hapo sokoni na wakirudi wanakuta vitu vyao kama walivyoviacha. kitu kingine kilichonifurahisha ni jinsi muda wa kuswali ukifika wanafunga hata Bank yao.
Nadhani lazima kuna wengine ambao pia hawajawahi kuisikia nchi hii.
1 comment:
Yeah, it is true, Somaliland exist and it is peacefull. Somaliland na Somalia zilikua nchi mbili tofaute, somaliland ilitawalia na Muingereza, na somalia ilitawalia na mtaliani. Raia wa Somaliland ni wastarabu, wana pend maendeleo, napia wana penda sana na kuthamini amani na utulivu. Somaliland na somalia ziliungana kama vile Tanganyika na Zanzibar zilivyo ungana, lakini raia wa Somalia wana penda ulaghai, vita na kumwaga damu ya wenzao. Ndio maana Somaliland wame amua kujitenga au kurudisha uhuru wao walio upoteza. I hope i have enlightened you a little bit, please inform many Tanzanians the difference between Somaliland and Somalia, thanks.
Post a Comment