KIKUNDI cha Sanaa za Maigizo ya Luninga nchini maarufu kama 'Ze Komedi' kimeulalamikia uongozi wa East Afrika Television (EATV) kwa kuwazuia kutumia majina na uhusika wa uigizaji waliokuwanao katika kituo kingine cha TV kwa madai kuwa ni hati miliki yao.Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ze Komedy Production, Isaya Mwakisyala alisema uamuzi wa Cosota kukubaliana na ombi la EATV kuwa Ze Komedy ni mali yao katika barua walioiandika Juni 9 na kujibiwa na Cosota Juni 10 kuwa ni mali yao si sawa kwa kuwa wao ni kikundi kinachojitegemea."Hatukuanzishwa na EATV bali tulikuwa ni waigizaji kipindi kirefu kabla hata hatujaonekana huko, kinatushangaza na kustaajabisha kitendo cha EATV kudai kuwa Ze Komedy ni mali yao, sisi tuanchosema tutaendelea kuwa huru na kubakia vile vile katika uigizaji huo kama kawaida," alisema Mwakisyala.Alisema mkataba wa uhalali wa kumiliki kikundi cha Ze Komedy waliupata Julai Mosi mwaka 2007 kwa cheti halali baada ya kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) tofauti na EATV ambao wanadai kupewa umiliki wa Ze Komedy Juni 30 mwaka huu.Alisema endapo kutatokea kutoelewana kokote baada ya uamuzi wao wa kuingia mkataba na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1) ambao uhamasishaji wa matangazo ulianza jana, watakwenda kumuona Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na ikishindikana watafika kwa Waziri Mkuu na hatimae kwa Rais.Hata hivyo kurushwa kwa vipindi vya kundi hilo TBC1 kutaanza baada ya wiki mbili zijazo kutokana na safari ya kundi hilo nchini Uingereza baada ya kuahirisha ya kwanza nchini Afrika Kusini kutokana na ghasia zilizokuwapo nchini humo.
1 comment:
Wameishiwa hao EATV. yote hiyo ni Hasira. Mtajiju
Post a Comment