mimi ni mpenzi wa tamthilia hizi za kutoka huko kwa wenzetu, leo ngoja niongelee nilichojifunza kwenye thamthilia hii ya LALOLA. kuna vijana wawili yaani msichana na mvulana wote wako ofisi moja lakini hawana marafiki basi kila mmoja akaamua kutafuta mwenza kwa kupitia mtandao, wakaanza kuchat huku kila mmoja akimdanganya mwenzio kuhusu jina lake na sehemu ya kazi ambayo ameajiriwa. basi wakaamua kubadilishana picha na kila mmoja akatuma picha ambayo sio ya kwake wote na kila mmoja anaamini kuwa kweli amepata mwenza. kwa uhondo zaidi angalia Tamthilia hii kupitia ITV.
No comments:
Post a Comment